May 16, 2021


 NAHODHA wa Azam FC, Agrey Morris amesema kuwa walitumia nafasi kwenye mchezo wao wa jana Mei 15 mbele ya Azam FC  na kupata ushindi.

Azam FC ilishinda mabao 2-1 Uwanja wa Azam Complex na kuwapa pointi tatu mazima mbele ya KMC ambao kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza Uwanja wa Uhuru ubao ulisoma KMC 1-0 Azam FC.

Mbele ya Kocha Mkuu, George Lwandamina vijana wake wakiongozwa na Prince Dube waliweza kulipa kisasi na kusepa na pointi zao.

Morris amesema:"Siwezi kusema kwamba ni mimi peke yangu niliyeipa ushindi timu hapana ila efforts, (jitihada) ambazo zilionyeshwa kwa wachezaji wote pia ninawapongeza wachezaji wa KMC mechi ilikuwa nzuri na ushindani wa wazi.

"Hamna mpira ambao tangu unaanza unashambulia wewe hapana, kila timu inapambana kupata matokeo. Tunachotakiwa kwa sasa ni kujipanga kwa ajili ya mechi zetu ili kupata matokeo,".

Kwenye msimamo, Azam FC ipo nafasi ya tatu ina pointi 57 ikiwa imecheza jumla ya 29 na kibindoni ina pointi 57 huku KMC ikibaki nafasi ya tano na pointi zake ni 41.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic