BRENDAN Rodgers,Kocha Mkuu wa Leicester City amesema kuwa taji la FA kiuhalisia lilikuwa linahitajika na timu, hivyo kushinda kwao wametimiza malengo yao kwa asilimia 100.
Huu unakuwa ni ubingwa wa kwanza wa FA kwa Leicester City kuutwaa baada ya ubao wa Wembley kusoma Chelsea 0-1 Leicester City katika fainali ya FA usiku wa kuamkia leo.
Bao pekee la ushindi lilipachikwa na kiungo Youri Tielemans dakika ya 63 ambalo lilikwenda katika eneo la kona iliyomshinda kipa wa Chelsea Kepa Arrizabalaga.
Rodgers amesema kuwa amefurahishwa na ushindi huo ambao wamepata kwa kuwa walikuwa wanalihitaji kombe hilo.
"Kombe ambalo tumelipata tulikuwa tunalihitaji hivyo kushinda kwetu ni furaha na ninawapongeza wachezaji kwa kucheza kwa juhudi na kupata ushindi katika mchezo ambao ulikuwa na ushindani mkubwa," .
0 COMMENTS:
Post a Comment