SALUM Kihimbwa nyota wa Mtibwa Sugar amesema kuwa wapo sehemu mbaya sana kwa sasa ndani ya Ligi Kuu Bara hivyo wana kazi ya kujinasua hapo walipo.
Ushindi wao wa jana mbele ya Tanzania Prisons, Uwanja wa Jamhuri kwa bao 1-0 unawafanya wafikishe jumla ya pointi 31 baada ya kucheza mechi 29.
Ni Kihimbwa mwenyewe alipachika bao hilo kwa kichwa dakika ya 5 akimalizia pasi ya George Makang'a na kuwafanya wapate pointi tatu.
Kwenye msimamo wa ligi Mtibwa Sugar ipo nafasi ya 14 haijawa kwenye mwendo mzuri msimu huu kutokana na kupata matokeo ambayo hayawafurahishi wachezaji.
Nyota huyo amesema:"Ninamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuipatia pointi tatu timu yangu ila tupo katika nafasi mbaya tena sana kwa sasa.
"Kikubwa kilichobaki ni kuona kwamba tunashinda mechi zetu zijazo na tutapambana ili kupata matokeo chanya hivyo mashabiki watupe sapoti," amesema.
0 COMMENTS:
Post a Comment