MCHEZO wa Ligi Kuu Bara kati ya Azam FC dhidi ya KMC utachezwa saa 1:00 usiku badala ya saa 10:00 jioni.
Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa KMC, Christina Mwagala amesema kuwa muda wa mchezo huo umebadilishwa tofauti na awali.
Mwagala amesema:"Mechi yetu ya KMC dhidi ya Azam FC umebadilishwa muda kutoka saa 16:00, (10:00) jioni tena ni saa 19:00, (1:00) usiku, Uwanja wa Chamazi. Nawatakia sikukuu njema,".
Mchezo wa kwanza walipokutana Uwanja wa Uhuru, ubao ulisoma KMC 1-0 Azam FC hivyo leo utakuwa na ushindani mkubwa kwa timu zote mbili kusaka pointi tatu.
Kwenye msimamo KMC ipo nafasi ya 5 na pointi zake 41 inakutana na Azam FC iliyo nafasi ya tatu na pointi 54,
Wakigona oooh busara itumike haya mambo yataisha lini huu ubabaishaji
ReplyDeleteKwani waligoma au walikimbia kichapo
ReplyDeleteVipi wamekubali na wao pia wangegoma kama wajuwaji wa pale
ReplyDeleteAcheni ujinga na uvivu wa kufikiri!Hao bodi ya ligi na TFF wanacheza na saikolojia za watu ili kuhalalisha upuuzi walioufanya kwenye mechi ya watani wa jadi.
ReplyDeleteYanga vs Namungo game ya kwanza ilirudishwa nyuma ikachezwa saa nane badala ya saa kumi, walikuwa wanacheza na saikolojia ya nani??
ReplyDeleteKwa wajuaji wa soka shida hakuna ila kwa wale wa ziwani wangekimbia uwanjani kwa kusoma kanuni zao bila ya kumaliza vifungu vya sheria
ReplyDelete