May 15, 2021


 TAARIFA zilizoripotiwa na vyombo vya habari vya Hispania zinaeleza kuwa Kocha Mkuu wa Klabu ya Real Madrid, Zinedine Zidane amethibitisha kuwa ataondoka klabuni hapo mara baada ya kumalizika kwa msimu huu hata kama atachukua ubingwa wa Ligi Kuu ya Hispania LaLiga.

 

Madrid ambao walisepa na ushindi mbele Granada na kufanikiwa kuondoka na pointi tatu kwa kuifunga bao 4-1 wakiwa ugenini, kwa sasa wapo katika nafasi ya pili ya msimamo wa La Liga wakiwa na pointi 78 nyuma ya Atletico Madrid ambao wana pointi 80 na michezo miwili imesalia kumalizika kwa ligi hiyo.


Zidane (48) akiwa Madrid ameshinda mataji mawili ya La liga na mataji matatu ya UEFA Champions League kwa misimu minne ambayo ameitumikia klabu hiyo lakini ameamua kuondoka klabuni hapo baada ya mechi yao ya mwisho ya ligi dhidi ya Villarreal itakayopigwa Mei 23, Santiago Bernabeu.

 

Zidane atakuwa chagua la kwanza la Juventus na timu ya taifa ya Ufaransa iwapo watafanya mabadiliko ya kocha baada ya Fainali za Euro zinazotarajiwa kuanza Juni 11.


Rais wa Madrid, Florentino Perez yupo katika wakati mgumu kusaka mbadala wa Zidane ambapo inaelezwa anataka kumpandisha Kocha Raul kuchukua mikoba ya Zizzou ama atamchukua tena kocha Max Allegri.

 

Zidane amesema anahisi hayuko kwenye moyo wa Perez na hata kama atachukua taji la La Liga kwa mara ya tatu, rekodi ambayo atakuwa ameiweka ya kurudisha kombe la La Liga kwa misimu miwili mfululizo.

 

Zidane ameingia kwenye vichwa vya habari baada ya kutofautiana na mchezaji wake, beki kisiki Marcelo raia wa Brazil baada ya kumuacha katika kikosi chake kilichocheza na Granada huku ikielezwa kuwa wawili hao hawana mahusiano mazuri klabuni hapo kwa sasa.


Marcelo atamaliza mkataba wake mwishoni mwa msimu huu. Marcelo anasema Zidane amekuwa mtu wa kukosoa sana katika mazoezi wakati akizungumza na timu yake kuhusu ushindi wa mechi zake, lakini pia alizungumza mbele ya meneja wa timu kuhusu kuamua kumuacha Marcelo na kumchukua kinda wa miaka 19, Miguel Gutierrez kuanza.

 


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic