ROBO fainali ya kwanza iliyowakutanisha MC Alger ambao walikuwa nyumbani dhidi ya Wydad Casablanca anayochezea Mtanzania Simon Msuva ulikamilika kwa sare ya kufungana bao 1-1.
Robo fainali hiyo katika Ligi ya Mabingwa Afrika ilichezwa Uwanja wa du 5 Juillet na Waydad walikuwa katika ubora wakiongoza katika umiliki wa mpira na mashuti yaliyolenga langoni.
Ni Yahya Jabrane mshikaji wake Msuva alipachika bao kwa mkwaju wa penalti dakika ya 66 na lilisawazishwa na Miloud Rebiai dakika ya 83.
Wydad walipiga jumla ya pasi 462 na MC Alger walipiga jumla ya pasi 401 huku kwa upande wa umiliki, MC Alger walikuwa na asilimia 47 na Wydad asilimia 53.
Kwa upande wa mashuti jumla 12 kwa Wydad na matatu yalilenga lango huku MC Alger wakipiga mashuti 8 na mawili yalilenga lango na kwenye mchezo huo Msuva alianza kikosi cha kwanza.
Mshindi atakayesonga hatua ya nusu fainali atapatikana kwenye mchezo wa robo fainali ya pili inayotarajiwa kuchezwa Mei 22.
0 COMMENTS:
Post a Comment