May 19, 2021

 


BARAZA la Sanaa la Taifa (BASATA) kushirikiana na vikundi viwili vya sanaa wameandaa tamasha la wanafunzi 250 kutoka shule tano za msingi litakalofanyika Alhamisi ya Mei 20 kwenye ukumbi wa BASATA, Dar es Salaam.

Mratibu wa tamasha hilo, Ramadhani Maneno (Pendapenda) amesema lengo la Tamasha hilo ni kukuza utamaduni wa mtanzania kwa watoto huku ujumbe ukiwa ni kupiga vita umasikini dhidi ya Corona.

Pendapenda ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kikundi cha Sanaa cha Safi Theatre kitakachoshiriki tamasha hilo amezitaja shule zitazoshiriki tamasha hilo ni Blessed Hill ya Kitunda, Shule ya Msingi Umoja ya Ilala na Shule ya viziwi ya St. Augustino ya Buguruni.

Mratibu huyo amesema kikundi kingine ni shule ya msingi ya Joyfull kutoka Bagamoyo mkoa wa Pwani na mgeni rasmi ni Diwani wa Kata ya Buguruni, ambaye pia ni Katibu wa Madiwani wa Wilaya ya Ilala, Busoro Pazi.

Amesema tamasha hilo pia litasidikizwa na vikundi maarufu vya sanaa vya Safari Theatre, Hisia Theatre, Happy Centre, Baba Watoto, Tatanisha Dance Crew, Butterfly Lion Group, Kibasila Sanaa Group vyote vya Dar es Salaam.

Pendapenda amesema zawadi mbalimbali zitatolewa kwenye tamasha hilo za ngao na kila kikundi kitakachoshiriki kitapewa cheti.




0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic