May 19, 2021


 ILIKUWA ni safari ndefu kwa timu kupambana kushinda ndani ya Ligi ya Wanawake Tanzania na mwisho wa siku kila mmoja ameweza kupata kile ambacho alikipata.

Msimu huu wa 2020/21 umekuwa ni wa tofauti kutokana na ushindani ambao ulikuwa upo kwa timu zote shiriki na mwisho wa siku kila timu imepata kile ilichokuwa ikihitaji.

Ni Simba Queens ambao wametwaa ubingwa huo kwa tofauti ya pointi moja na watani zao wa jadi Yanga Princes hivyo nina amini kwamba msimu ujao ushindani utakuwa mkubwa.

Kwa kuwa wamemaliza mapema basi itapendeza pia Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF) kwa kushirikiana na wadhamini pamoja na wadau kuwapa zawadi zao mapema ili maisha mengine yaendelee.

Zawadi ambazo watapewa haina maana kwamba ni jambo kubwa kwao bali ni kumbukumbu ambayo itaishi na kuwafanya wazidi kupambana kufikia malengo yao wakati ujao.

Tunaona kwamba mfungaji bora pia amepatikana huyu naye anastahili pongezi huku wale wenzake ambao walikuwa naye pamoja kuzidi kujifunza ili kuleta ushindani kwa wakati ujao.

Zile zengwe ambazo zimekuwa zikisisika hasa kwa upande wa zawadi ziwekwe kando na badala yake yawepo maboresho zaidi yatakayowafanya wazidi kuwa bora.

Ni jambo la kupongeza timu zote shiriki pamoja na zile ambazo zilikwama kumaliza ligi kutokana na matatizo ya ukata.

Hapo kuna suala la kulitazama kwa ukaribu kwa upande wa masuala ya fedha ambazo zimekuwa zikikwamisha mipango ya timu nyingi.

Kila timu ina nafasi ya kufanya vizuri ikiwa itajipanga kwa umakini hivyo wakati ujao nina amini kwamba kutakuwa na ushindani mkubwa na kila mmoja atapata kile ambacho anastahili.


 


 


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic