BREAKING: TAARIFA iliyotumwa na Bodi ya Ligi Tanzania, (TPLB) leo Mei 16 ambayo ni ratiba ya Ligi Kuu Bara imeonyesha tarehe mpya ya mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya Simba na Yanga ambao uliyeyuka mazima Mei 8, Uwanja wa Mkapa kutokana na Yanga kugomea mabadiliko ya muda.
Muda wa awali wa mchezo huo ulipangwa majira ya saa 11:00 ila muda mfupi kabla ya mchezo ratiba ilibdilishwa na kupelekwa mpaka saa 1:00 usiku jambo ambalo Yanga waligomea.
Yanga iliweka wazi kwamba ni lazima Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania, (TFF) kufuata kanuni kwa kuwa mpango huo ulikuwa ni kinyume na taratibu kuhusu kubadilisha muda.
Sasa watani hao wa jadi wanatarajiwa kukutana tena Uwanja wa Mkapa, Julai 3, Uwanja wa Mkapa saa 11:00 jioni.
Upumbavu hiyo tarehe bingwa ashajulikana yaani mwezi wa sita wote wasikutane
ReplyDeleteBingwa atakuwa Nani?
DeleteTulia kama unanyolewa wewe. Siku hiyo ndipo wanaume watakabidhiwa kombe lao la ubingwa wa nne (4) mfululizo.
ReplyDeleteHivi utopolo mna mawazo ya ubingwa
DeleteKwahiyo target ilikua tarehe isiogawanyika kwa 2? Wabadilishe na ta Keizer Chief pia.
ReplyDeleteAhahahah
Bodi ya ligi na TFF hawana tofauti na Bongo movie.
ReplyDeleteShida ya kuwaogopa wanasiasa kwa sababu ya vyeo vyao matokeo yake ligi inaendeshwa kama bonanza la vikundi vya wanywaji toka bar mbali mbali
Karia na genge lake TFF imeshawashinda wangeliachia ngazi kabla ya kupatwa aibu kubwa.
ReplyDeleteNaona ni sawa tu na wakati uleee, TFF ilivyowashinda Malinzi na genge lake!!
ReplyDeleteKwani mlipokimbia uwanjani mlitaka ipangwe tarehe ipi?
ReplyDeleteNa safari hii tena utopolo watakimbia tena
ReplyDeleteUmewekwa Mpaka mwezi wa saba ili uwe msaada kwa wachezaji wa matopolo wapate wakati Wa kutosha ili majruhi wao wapone wasije kupata visibabu kuwa mastaa wao wengi hawajiwezi
ReplyDelete