COASTAL Union ya Juma Mgunda leo Mei 16 imekubali kushuhudia ubao wa Mkwakwani Tanga ukisoma Coastal Union 0-1 Polisi Tanzania.
Ni Deusdedit Cosmas alipachika bao la ushindi dakika ya 52 na kuwafanya Coastal Union wasiwe na chaguo baada ya kuyeyusha pointi tatu mazima.
Malale Hamsini, Kocha Mkuu wa Polisi Tanzania amewashuhudua vijana wake wakisepa na pointi tatu muhimu.
Vijana wa Mgunda watajilaumu wenyewe kwa kuwa walipata penalti iliyopigwa na Haji Ugando ambaye alikosa baada ya kipa kuikoa penalti hiyo.
Pia alipata nafasi ya wazi akiwa ndani ya 18 Ugando bahati haikuwa yake kabla ya kuupiga mpira aliteleza na kupoteza nafasi hiyo.
Matokeo hayo yanaifanya Coastal Union kubaki na pointi zake 33 ikiwa nafasi ya 13 na Polisi Tanzania wanafikisha jumla ya pointi 41 nafasi ya 6.
0 COMMENTS:
Post a Comment