KIKOSI cha Yanga Princes leo Mei 16 kimefunga pazia la Ligi ya Wanawake Tanzania kwa ushindi wa mabao 6-0 dhidi ya Alliance Girls kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Uhuru.
Ni mshambuliaji wao namba moja ambaye anafanya vizuri pia kwenye timu ya taifa ya Tanzania ya Wanawake, Aisha Masaka alitupia mabao matano.
Alifunga hat trick ya mapema ndani ya dakika 15 na kuongeza nguvu kwa timu yake hiyo ambayo inanolewa na Kocha Mkuu, Edna Lema kusepa na pointi tatu muhimu.
Ni Clara Luvanga alipachika bao moja kati ya sita na kukamilisha ushindi wa mabao 6-0 kwa Yanga.
Kikosi hicho kimeleta ushindani mkubwa ambapo baada ya kumaliza mchezo huo walianza kuvutia kasi mchezo wa watani zao wa jadi, Simba Queens ambao walikuwa wamebanwa mbavu na Baobab Queens katika mchezo wao wa mwisho uliochezwa Uwanja wa Jamhuri, Dodoma mpaka dakika ya 87.
Ni Asha Djafar alipachika bao la ushindi lililotibua furaha ya Yanga Princes kusubiri kutwaa ubingwa kwa mara ya kwanza.
Kwenye msimamo Yanga Princes ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 53 huku Simba Queens ikiwa na pointi 54 zote zimecheza jumla ya mechi 19.
0 COMMENTS:
Post a Comment