KOCHA Mkuu wa Simba, Didier Gomes amesema kuwa jambo lolote linaweza kutokea kwenye mpira hivyo bado wana matumaini ya kupata matokeo kwenye mchezo wao dhidi ya Kaizer Chiefs.
Jana, Mei 15 Simba ilikubali kichapo cha mabao 4-0 dhidi ya Kaizer Chiefs katika mchezo wa robo fainali ya kwanza Uwanja wa FNB Soccer City, Afrika Kusini.
Ina kibarua cha kusaka ushindi kwenye robo fainali ya pili itakayochezwa Uwanja wa Mkapa, Mei 22.
Gomes amesema:"Hatujafurahia matokeo, jambo lolote linawezekana na tuna matumaini ya kupata matokeo kwa kuwa bado tuna mchezo.
"Ila ili kama tunataka kupata matokeo ni lazima tuwe bora zaidi,".
Ikiwa Simba italazimisha sare Uwanja wa Mkapa safari yao itakuwa imeishia hatua ya robo fainali.
Mungu kaumba siku furaha siku huzuni
ReplyDeleteNa hapana shaka furaha itarejea tena Unyamani
ReplyDeleteJipeni tumaini hivyo hivyo ili Simba ishinde ni lzm yafanyike mambo mkakati kweli kweli sio kuonfelea ushabiki tu. Kuanzia nje ya uwanja hata kabla ya uwanja mikwala mbuzi na fisi lzma itumike kabla ya mechi vinginevyo kwishnei. Maana Kaizer hawana mpira wa magazetini wala hawana maufundi meeengi ila ukizingua tu pini
ReplyDeleteTutatafuta paka kwa garama yoyote. Mbona vita alikula 4 huku
ReplyDeleteKuwahonga marefa itakuwa vigumu na TFF kuwabeba kama walivyozoea haitowrzekana lakini wanaweza wakafanya mambo mawili ambayo yalishawahi kuwasaidia:
ReplyDelete1. Kuwabambikizia wachezaji hatari wa Kaizer Chiefs ugonjwa wa Corona siku watakayowasili ili wasiruhusiwe kucheza kama ilivyotokea kwa Wasudan.
2. Kupuliza dawa za kunyongonyeza kwenye chumba cha kubadilishia nguo cha Kaizer Chief ili walewe na kucheza chini ya kiwango.
La sivyo uwezekano wa kupindis meza ni mdogo.
Ukweli tupu.
DeleteAngalia ukweli utakuponza.
DeleteSasa hivi kila timu iko makini, wanajua uozo wote uliojitokeza awali, ndio maana jana kaizer kamaliza hame kumpa mtu 4G. Akija huku ana defence tu na kupata goli la ugenini..
Hakuna miujiza uwanjani ndg, msproo wote simba, dakika 90 shoot on target 1.
Au unataka magoli ya penalt?
Au na hiyo mechi ya marudiano muongee na TFF ili waiairishe kama ile ya YANGA mapaka fc nyie
ReplyDelete