May 28, 2021



KOCHA msaidizi wa kikosi cha klabu ya Azam, Vivier Bahati amefunguka kuwa mshambuliaji wao, Prince Dube kwa sasa anaendelea vizuri baada ya juzi kushindwa kumaliza mchezo wao wa robo fainali dhidi ya Rhino Rangers kutokana na kupata maumivu ya tumbo.

Dube alipata changamoto hiyo dakika ya saba ya mchezo na kulazimika kutolewa uwanjani na nafasi yake kuchukuliwa na mshambuliaji raia wa Zambia, Obrey Chirwa ambaye alifanikiwa kufunga bao moja katika ushindi wa mabao 3-1 walioupata Azam dhidi ya Rhino.

Kutokana na ushindi huo Azam sasa wanatarajiwa kuwavaa Simba, katika mchezo wa nusu fainali itakayopigwa kwenye uwanja wa Majimaji, Songea mkoani Ruvuma kati ya Juni 24, hadi 28, mwaka huu.

Akizungumzia hali ya mshambuliaji huyo kocha Bahati amesema: “Tunamshukuru Mungu kwa matokeo ya ushindi wa mabao 3-1 ambayo tuliyapata dhidi ya Rhino Rangers katika mchezo wetu wa hatua ya robo fainali, ulikuwa mchezo mgumu na tulipoteza nafasi nyingi za kufunga mabao lakini jambo zuri ni kwamba tumefanikiwa kufika hatua ya nusu fainali.

“Kwa bahati mbaya mshambuliaji wetu, Prince Dube hakuweza kumaliza mchezo lakini niwatoe hofu kuwa, Dube hakupata majeraha yeyote, bali alipata mchafuko wa tumbo na akapatiwa matibabu na kwa sasa yupo sawa kutumika katika michezo yetu ijayo,”

 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic