KOCHA mkuu wa klabu ya Namungo, Hemmed Morocco amekiri kuwa wanakabiriwa na mchezo mgumu dhidi ya Simba utakaopigwa kesho mkoani Lindi.
Namungo na Simba wanatarajiwa kukutana kwenye mchezo wao wa kiporo unaotarajiwa kupigwa kesho Jumamosi katika uwanja wa Majaliwa mkoani Lindi, ambapo mchezo huo utakuwa wa kwanza kwa timu hizo mbili kukutana msimu huu.
Tangu kupanda kwao Ligi Kuu Bara, Namungo wamekuwa na wakati mgumu mbele ya Simba ambapo katika michezo yao mitatu waliyokutana mpaka sasa, Simba wamefanikiwa kuibuka na ushindi katika michezo miwili huku mchezo mmoja ulioisalia ukimalizika kwa suluhu.
Akizungumzia maandalizi yao, Kocha Morocco amesema: “Tunashukuru baada ya kufanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Gwambina katika mchezo wetu uliopita wa Ligi Kuu Bara, tunakabiliwa na mchezo mgumu wa Jumamosi (kesho) dhidi ya Simba, ambao tunajua wazi kuwa ni miongoni mwa timu bora kwa sasa.
“Lakini licha ya kutambua kuwa
tunakwenda kukutana na wapinzani wagumu bado tumejiandaa kupambana, ili kuweza
kupata matokeo mazuri katika mchezo huo na kuzidi kumaliza katika nafasi nzuri
zaidi kwenye msimamo wa ligi."
Cyeye tu team zote zinaweweseka dhidi ya simba
ReplyDeleteNi kweli, ndo maana wengine wanakimbia ili kuepuka kipigo
Delete