UONGOZI wa Yanga umekiri kuwa ubora wa
Mkata Umeme wao Mkongomani, Mukoko
Tonombe umekuwa ukizivutia klabu nyingi
kubwa barani Afrika, ambazo zimeonekana
kuhitaji huduma ya kiungo huyo.
Mukoko ambaye amebakisha mwaka mmoja tu
katika mkataba wake na Yanga, ameonekana
kuzivutia baadhi ya klabu kubwa wakiwemo wababe wa soka kutokea nchini Guinea, Horoya
ambao wanatajwa kuweka dau la zaidi ya Sh
milioni 400 za Kitanzania kwa ajili ya kupata
huduma yake.
Mukoko akiwa katika msimu wake wa kwanza
tu ndani ya kikosi cha Yanga, amefanikiwa
kuhusika katika mabao nane akifunga mabao
manne na kuasisti mabao manne mpaka sasa.
Mkurugenzi wa Mashindano wa Yanga, Thabit
Kandoro, alisema: “Siyo jambo jipya sana
kusikia mchezaji kama Mukoko Tonombe
anawindwa kusajiliwa na timu kubwa kutokana
na ubora alionao kwa sasa, na hasa ukizingatia
kuwa ni miongoni mwa wachezaji wachache
walio na nafasi kwenye kikosi cha timu ya taifa
ya Congo.
“Hivyo kama uongozi wa Yanga tunaelewa
kuwa kuna timu nyingi za nje ya nchi ambazo
zinahitaji huduma ya Mukoko, ambazo
nisingependa kuzitaja lakini hatujapata ofa
yoyote mpaka sasa.”
0 COMMENTS:
Post a Comment