May 13, 2021

 


OFISA Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa kwa namna anavyokitazama kikosi cha Yanga kinachonolewa na Kocha Mkuu, Nassredine Nabi anakubali uwezo wa nyota wengi ikiwa ni pamoja na Feisal Salum.

Manara amesema kuwa wengi wanaibeza Yanga wakidhani haina wachezaji wazuri jambo ambalo sio kweli kwani kuna wachezaji wazuri ambao wanaweza kupata nafasi ndani ya kikosi cha Simba kinachonolewa na Didier Gomes.

“Unajua wengi hawajui kwamba Yanga ina wachezaji wazuri ambao wengine kati yao wanaweza kucheza kikosi cha kwanza Simba angalau wakagombania namba ikiwa ni pamoja na Fei Toto.

“Fei Toto anajuhudi na anakipaji ambacho ukiangalia unaona kwamba anaweza kugombania namba Simba. Kugombania namba Simba sio mchezo, napenda namna anavyocheza,” amesema Manara.

Ndani ya kikosi cha Yanga kwa msimu wa 2020/21 katika Ligi Kuu Bara, Fei amecheza jumla ya mechi 23 kati ya 27 na kutumia dakika 1,935 na alitupia bao moja mbele ya Mwadui FC.



8 COMMENTS:

  1. Manara anakuuma halafu anakupuliza

    ReplyDelete
  2. Fei Toto hawezi kuingia first eleven ya Simba coz hawezi muweka bench Thadeo Lwanga Wala Mkude labda at least angesema Mukoko Tonombe,huo ndiyo ukweli

    ReplyDelete
    Replies
    1. Acheni upuuzi nyie kwani kawaomba mumsajili?

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic