May 14, 2021

 LICHA ya kwamba kwa sasa ndani ya Ligi Kuu Bara mtupiaji namba moja ni Prince Dube wa Azam FC,  Kocha Mkuu wa Simba, Didier Gomes amesema kuwa nyota wake Kagere atamaliza akiwa ni namba moja.


Kagere ni mfungaji bora kwa misimu miwili mfululizo,  aliibuka mfungaji bora msimu wa 2018/19 akiwa na mabao 23 na msimu wa 2019/20 akiwa na mabao 22.



Msimu huu wa 2020/21 amekutana na chuma, Dube ambaye anampa presha akiwa ni mtaalamu wa kucheka na nyavu ndani ya Azam FC,  ametupia mabao 12.


Kagere yeye msimu huu mpaka sasa ametupia jumla ya mabao 11 na mshikaji wake John Bocco ana mabao 10 ndani ya Ligi.


Gomes amesema:"Ninawaamini wachezaji wangu hasa katika safu ya ushambuliaji imani yangu ni kwamba watamaliza wakiwa juu katika suala la ufungaji hilo sina mashaka nalo.


"Suala la muda na utulivu kwao litawafanya wafikie malengo yao ipo wazi ushindani mkubwa nao wanashindana pia," .


Kwa sasa Simba ipo Afrika Kusini kwa ajili ya maandalizi ya mchezo dhidi ya Kaizer Chiefs ambao ni robo fainali ya kwanza Ligi ya Mabingwa Afrika,  unatarajiwa kuchezwa Mei 15.

1 COMMENTS:

  1. Yaani TFF wanashida gani, imeruhusu simba kwenda SA mapema kiasi hicho ilihali wanavipolo vya mechi kibao.siwangecheza halafu wakaondoka. TFF ni jipu kubwa na limeiva linafaa kutumbuliwa.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic