NAHODHA msaidizi wa Yanga, Bakari Mwamnyeto ambaye ni beki wa kati amesema kuwa bado timu hiyo inayo nafasi ya kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Jana Mei 15 ubao wa Majaliwa baada ya dakika 90 ulisoma Namungo 0-0 Yanga na kuwafanya wagawane pointi mojamoja.
Sare hiyo inawafanya Yanga wafikishe jumla ya pointi 58 baada ya kucheza mechi 28 huku Namungo FC ikiwa nafasi ya 10 na pointi zake ni 36 baada ya kucheza jumla ya mechi 26.
Mwamnyeto amesema:-"Mechi ilikuwa ngumu lakini tunashukuru Mwenyezi Mungu tumetoka sare.
"Bado tunao uwezo wa kuchukua ubingwa, tumetoka sare hatujapoteza, tunaweza kupata pointi tatu za JKT Tanzania tukakaa vizuri,".
Kwa sasa bingwa mtetezi ni Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes ikiwa imekusanya pointi 61 baada ya kucheza mechi 25.
Msikate tamaa ingawa wa kale walisema, ulimi hauna mfupa na mdomo jumba ya maneno
ReplyDeleteMwamyeto nae keshakuwana fikira za Kiyanga
ReplyDeleteAcheni ndoto zisizotimilika.
ReplyDeleteWANA JAMBO LAO MWAKA HUU WAMESEMA
ReplyDelete