May 18, 2021


 KIPA wa Klabu ya Arsenal, Bernd Leno amesema kuwa atabaki ndani ya kikosi hicho kwa kuwa hana mpango wa kuondoka.

Imekuwa ikielezwa kuwa Leno ana mpango wa kuondoka ndani ya Uwanja wa Emiretes ili akapate changamoto mpya kwa kuwa anahitaji kwenda kwenye timu itakayoshiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Raia huyo wa Ujerumani amesema kuwa anafurahi kuwa ndani ya Arsenal hivyo ataendelea kubaki hapo.

Wiki iliyopita iliripotiwa kwamba yeye pamoja na nyota wengine watano hawafurahii maisha ya Arsenal kutokana na mwendo wake kutokuwa bora.

Kipa huyo amesema:"Sihitaji kuondoka kwa sasa nitabaki hapa, ninafurahi kuwa hapa kwa sasa,". 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic