KOCHA mkuu wa kikosi cha klabu ya Simba, Didier Gomes juzi kwenye mazoezi ya kikosi cha klabu ya hiyo kunachojiandaa na mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Kaizer Chiefs aliwarudisha kwenye kikosi cha kwanza nyota wa kikosi hicho, John Bocco, Mzamiru Yassin na Bernard Morrison.
Kati ya nyota hao watatu ni, John Bocco pekee ndiye
aliyecheza mchezo wa kwanza Afrika kusini ambapo aliingia kuchukua nafasi ya
Luis Miquissone dakika ya 84 ya mchezo, huku Morrison na Mzamiru wakishindwa
kuwa sehemu ya mchezo huo.
Katika mazoezi hayo ya Jumatano, Bocco, Mzamiru pamoja na
Morrison walivaa jezi za mazoezi ‘bibs’, ambazo pia zilivaliwa na wachezaji
wote waliocheza mchezo wa kwanza nchini Afrika Kusini na kupewa program maalum
dhidi ya kundi la wachezaji wengine wa akiba.
Kutokana na hali hiyo kuna uwezekano mkubwa nyota hao watatu
wakawa sehemu ya mchezo wa kesho, ikiwemo kuanza kwenye kikosi cha kwanza.
0 COMMENTS:
Post a Comment