PACIFIQUE Ndabihawenimana mwenye umri wa miaka 36, ndiye anatajwa kusimama kuamua vita ya kesho kati ya Simba dhidi ya
Kaizer Chiefs katika mchezo wa marudiano wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Mburundi huyo anatajwa kuwa na rekodi ya msimamo mkali na
urahisi wa kutoa adhabu ikiwemo kadi za njano na nyekundu, lakini pia kuhimili presha ya mchezo.
Simba Jumamosi iliyopita wakicheza ugenini katika uwanja wa
FNB (Soccer City), katika mchezo wa mkondo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika
walikumbana na kipigo cha mabao 4-0 ambayo yameweka rehani nafasi yao ya
kutinga nusu fainali ya michuano hiyo.
Simba ina deni kubwa la kuhakikisha wanashinda mchezo wa
kesho Jumamosi kwa tofauti ya mabao 5-0 ili kufufua matumaini yao ya kucheza
hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo.
Kujaribu sio kushindwa lakini kimsingi shughuli imekwisha!
ReplyDeleteKweli aisee, natamani sna tushinde lakini mlima huu ni mrefu sana, Kaizer wana mtaji mkubwa sana wa magoli. Let us wait and see. Walipofikia imba robo fainal mara mbili ni mafaniko makubwa sana ambayo hayazungumziwi sana, watu wanazungumzia tu kipigo cha goli nne.
DeleteMungu atusaidie tupindue matokeo ingawa mlima mrefu u never know
ReplyDeleteHakuna anayeichukia simba, ila watu wanachukia makelele na majigambo ya simba,
ReplyDeleteMnasema yanga wanaichukia simba lkn ukifanya utafiti kodogo utakuta haya gwambina wanapenda chief watinge nusu final.
Safari mlifika kwa kubebwa na Corona tu hna kitu buana
ReplyDelete