May 14, 2021

 


 MSHAMBULIAJIwa kimataifa wa Tanzania anayekipiga katika kikosai cha Wydad Casablanca cha Morroco, Simon Msuva amesema kuwa watafanya kila namna kuhakikisha wanapata matokeo mazuri katika mchezo wao wa leo Ijumaa wa ugenini dhidi ya MC Algers.

 

Wydad Casablanca, wanatarajiwa kuwa ugenini kucheza dhidi ya MC Algers katika mchezo unaotarajiwa kufanyika kwenye Uwanja Du 5 Juillet nchini Algeria.

 

Msuva alisema kuwa licha ya kukutana na timu ngumu na bora lakini mipango yao ni kufanya vizuri katika mchezo wao wa ugenini ili wamalize vizuri katika mchezo wa marudiano wakiwa nyumbani.

 

“Tunakutana na timu bora na ngumu, mipango yetu ni kufanya vizuri zaidi katika michuano hii, tunatakiwa kuchanga karata zetu vizuri hasa katika mchezo huu tukiwa ugenini ili mchezo wetu wa marejeano tumalize vizuri tukiwa nyumbani,” alisema mchezaji huyo.

 

Msuva katika Ligi ya Mabingwa msimu huu akiwa na Wydad Casablanca amefanikiwa kuifungia timu hiyo mabao mawili na kutoa asisti 1 ya bao katika michezo 6 aliyocheza.

Stori: Marco Mzumbe, Dar es Salaam

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic