May 16, 2021

 


BAADA ya dakika 90 kukamilika na ubao wa Uwanja wa FNB Soccer City kusoma Kaizer Chiefs 4-0 Simba, Ofisa Habari wa Simba,  Haji Manara amesema kuwa walicheza hovyo.

Kichapo hicho kinakuwa cha kwanza kwa Kocha Mkuu Didier Gomes kushuhudia idadi kubwa ya mabao kwa timu yake ikifungwa akiwa katika benchi baada ya kupokea mikoba ya Sven Vandenbroeck.

Haji Manara kupitia Ukurasa wake wa Istagram alisema:" Alhamdulillah. Tumefungwa na aliye bora usiku wa leo, tumecheza hovyo na tumefanya makosa mengi yaliyostahili adhabu hii.


"Life go on, (maisha lazima yaendelee) na still, (bado) tunazo dk tisini nyingine za kuamua,".


Mchezo wa robo fainali ya pili unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa, Mei 22 ambapo Simba wanapaswa kufunga mabao zaidi ya manne ili kusona mbele hatua ya nusu fainali.

10 COMMENTS:

  1. Hatua hii haina mipango na janjajanja za chumbani kama huko mlikotoka

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hatua hii ni tofauti sana na zile mechi za Lindi. War in Dar inakuja tena

      Delete
  2. Replies
    1. ili wabeba sana Wasouth. Simba bado ndio timu bora na ilicheza mpira bora zaidi kuwai kuchezwa South Afrika ukiachilia vigoli laini walivyofungwa na timu mbovu kuliko FC Platinam na kuliko AS vita. Simba itabadili matokeo sababu ndio timu bora zaidi kwa sasa katika Afrika. Tunachoangalia ni uwezo wa kucheza sio vigoli vya kubahatisha

      Delete
  3. There is no joy in victory if you don't run the risk of defeat. As usual with Simba, no blames against players and no talks of eviction of coach. Forget what happened and start afresh

    ReplyDelete
    Replies
    1. That's the football principle,let's wake up and move on

      Delete
  4. Ukiangalia mpira was Jana,Tshabalala ametucost Sana na nishawahi sema Simba inabidi itafute mbadala wake upesi,sababu Jana ametoa pasi mbili za mabao,hivyo bench la ufundi limtamfute mbadala wake upesi,goli moja ni uzembe wa kipa,Bado mipira ya cross inamsumbua Manula naye atafutiwe mbadala upesi,huo ndiyo ukweli na ukweli huponya

    ReplyDelete
  5. Nyie ndio hamchelewagi kusema paka alisababisha Simba akapindua matokeo tunaijua furaha yenu ni Kama Manisha ya funza kwa hiyo hamtupi tabu Kama timu yenu tu mlianza kulaumu marefa,mkaja kusema TFF wanawahujumu,mwisho mkaanza kulaumu wachezaji wenu wenyewe hatuwashangai mkitoa visingizio sijui huku Hamna mipango ndo Mana tumefungwa kwa sababu nyinyi Mpira kwenu ni siasa na ndo Mana huu ni mwaka wa nne mnamshabikia AS vita,Mara sijui Al Ahly wakati nyie wenyewe mna timu yenu utopolo halafu mnaajita wakubwa watu Kama nyinyi wiki mtatafuta sababu za kwa Nini Simba kapindua matokeo

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic