May 16, 2021


NYOTA wa zamani wa Yanga na timu ya taifa ya Tanzania, Ally Mayay amesema kuwa bado hajaelewa sababu ya mwamuzi kukataa bao la Yanga ambalo lilifungwa kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara, jana Mei 15 wakati ubao ukisoma Namungo 0-0 Yanga.

Katika mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Majaliwa, Yacouba Songne aliweza kupachika bao dakika ya 74 lilifutwa na mwamuzi jambo ambalo lilisababisha wachezaji wakiongozwa na nahodha Bakari Mwanyeto.

Mayay ambaye ni mchambuzi wa masuala ya mpira amesema:-"Kipindi cha kwanza na cha pili ilikuwa tofauti ambapo aproach,(mbinu) ya kipindi cha kwanza Yanga walikuwa wanacheza kama ambavyo Namungo walikuwa wanacheza katikati.



"Pia hali ya uwanja ilikuwa hairuhusu kuchezea mpira kama ambavyo ingekuwa kwenye Uwanja wa Mkapa ama Uwanja wa Azam Complex.

"Kipindi cha pili kulikuwa na mabadiliko na hata speed pia ilionekana kuongezeka na vitu ambavyo vilifanya zikapatikana faulo nyingi sana.

"Hata huo uthibitisho wa goli ambalo walifunga na unaona mpaka sasa maelezo bado mpaka sasa ya sababu za huo mpira kutoenda golini haieleweki

"Kama mpira ni offside,(kuotea) kona haina offside kwa sababu kona mpira sehemu ambayo inakaa ni sehemu ya mwisho ni goal line kwa hiyo hakuna definition, (maana) ya offside hivyo sababu nyingine mwamuzi anaweza kuelezea kwa nini hakuruhusu huo mpira kuwa ni goal mpira ulioingia wavuni," .

Ni Saido Ntibanzokiza ambaye alipiga kona hiyo na ikasindikizwa na kichwa cha nyota Tuisila Kisinda kabla ya kukutana na kichwa cha Yacouba ambaye alipachika bao hilo kwa kichwa ila lilifutwa.

8 COMMENTS:

  1. Ni maelekezo toka ngazi za juu......kwisha!!!!!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ala, kumbe hata lile goli la Onyango alilofunga kupitia kona dhidi ya Gwambina ilikua ni maagizo kutoka ngazi za juu

      Delete
    2. Kuna watu wanajitoa ufahamu tu! Goli la wazi la Onyango (kama lile) kule Gwambina lilivyokataliwa hakuna aliyesema ni "maelekezo toka ngazi za juu"!

      Delete
  2. Lile goli la mechi ya simba na Gwambina kukataliwa ilikuwa sawa

    ReplyDelete
  3. Sababu ni kuwa hilo lilikuwa bao la kuotea na wacheni malalamiko ya kila siku yasiyo na mana

    ReplyDelete
  4. Itakua sheria mpya, inayotumika na TFF kuwena Offside kwenye kupiga kona

    ReplyDelete
  5. Like gol mpigaj alimpiga kiwiko beki

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic