KIKOSI cha Simba Queens leo Mei 16 kimeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Baobab Queens na kuwafanya waweze kuwa mabingwa wa Ligi ya Wanawake Tanzania.
Ushindi huo ulipatikana kwa mbinde baada ya dakika 45 za mwanzo mabingwa hao watetezi wanaonolewa na Kocha Mkuu, Mussa Mgosi kukamilisha bila kuona lango la wapinzani wao na wala wao kufungwa.
Iliwachukua dakika 88 Simba kufunga bao la ushindi kupitia kwa Asha Djafar na kuwafanya wakamilishe dakika 90 na kusepa na pointi tatu muhimu huku kukiwa na zengwe la hapa na pale kutokana na wapinzani wao kuonekana wakilaumu maamuzi ambayo yalikuwa yanatolewa.
Ushindi huo unaifanya Simba kufikisha jumla ya pointi 54 ikifuatiwa na Yanga Princes yenye pointi 53 katika msimamo.
Ofisa Habari wa Simba Queens Monalisa amesema kuwa ni furaha kuwa mabingwa na yeye kwa sasa ni msemaji wa mabingwa.
Afadhali tumepoza kidogo ya jana
ReplyDelete