WANAJESHI wa mpakani, Biashara United leo Juni 15 wamelazimisha sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Namungo FC kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Karume, Mara.
Ni bao la kujifunga lililopachikwa na beki wa Biashara United,Lenny Kissu katika harakati za kuokoa shuti lililopigwa na Stephen Sey dakika ya 3 liliwekwa usawa dakika moja mbele na Denis Nkane dakika ya 4.
Matokeo hayo yanaifanya Namungo kusonga hatua moja mbele kutoka nafasi ya nane hadi nafasi ya tano na pointi 42 huku Biashara United ikiwa nafasi ya nne na pointi 46.
Kocha Mkuu wa Namungo FC, Hemed Suleman ameshuhudia vijana wake wakigawana pointi mojamoja na vijana wa Patrick Odhiambo.
0 COMMENTS:
Post a Comment