NEYMAR Jr, anatarajiwa kukiongoza kikosi cha timu ya Taifa ya Brazili katika michuano ya Copa America inayotarajiwa kuanza Jumapili.
Mabingwa hao watetezi watafungua panzia kwa mechi dhidi ya Venezuela.
Nyota huyo wa PSG aliukosa ubingwa wa Copa America 2019 kutokana na majeraha anarejea uwanjani pamoja na mshikaji wake Thiago Silva ambaye anatoka kwenye majeraha.
Hata hivyo kuna nyota wawili wa Brazil watakosekana katika michuano hiyo kutokana na majeraha ambao ni Dani Alves wa Sao Paulo na nahodha wa kikosi cha 2019 Phillippe Coutinho.
0 COMMENTS:
Post a Comment