June 26, 2021


 YACOUBA Sogne mshambuliaji wa kikosi cha Yanga jana aliendelea pale alipoishia kwenye mchezo wake wa Kombe la Shirikisho baada ya kufunga bao la ushindi lililoipekea timu hiyo hatua ya fainali ya Kombe la Shirikisho.

Wakati ubao wa Uwanja wa Alli Hassan Mwinyi ukisoma Biashara United 0-1 Yanga ilikuwa dk ya 22 akiwa ndani ya 18 Yacouba aliachia shuti kali lililomshinda mlinda mlango  James Ssetuba akitumia pasi mpenyezo ya Feisal Salum.

Hilo linakuwa ni bao lake la pili kwa Yacouba kufunga katika mchezo wa Kombe la Shirikisho kwa kuwa mara ya kwanza alifunga bao la ushindi kwenye mchezo ulioipeleka Yanga hatua ya robo fainali ilikuwa mbele ya Tanzania Prisons ambapo wakati huo alitumia pasi ya Said Ntibanzokiza.

Licha ya Biashara United kujitahidi kusaka bao kupitia kwa washambuliaji wao ikiwa ni pamoja na Deogratius Mafie ngoma ilikuwa ngumu kupenya kwenye ngoma ya Farouk Shikalo ambaye alikuwa imara.

Sasa Yanga wametinga hatua ya fainali ambapo wanasubiri mshindi wa mchezo wa leo Uwanja wa Majimaji kati ya Simba v Azam FC ambaye watakutana naye fainali.

Lengo la Yanga ni kusepa na taji hili la Kombe la Shirikisho ambalo lipo mkononi mwa Simba ambao nao wameweka wazi kwamba wanahitaji kusepa nalo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic