June 4, 2021

 


UMEONA kuhusiana na safu ya ushambuliaji ya 
Yanga, kuna taarifa kuna mshambuliaji anaweza kuondoka na inawezekana kuna mchezaji mwingine anaweza kuondoka.

Hadi sasa katika safu hiyo ya ushambuliaji ya Yanga, hakuna mchezaji ambaye amefikisha angalau mabao 11. Inawezekana kabisa katika wapya, Yacouba Songne anaweza kufikisha idadi hiyo kutokana na mwendo wake kuwa mzuri.

Kufikisha inawezekana, jiulize anaweza kuvuka idadi hiyo ya mabao na kumfanya kuwa ana idadi kubwa ya mabao ya kufunga kuliko aliyekuwa mfungaji bora wa msimu uliopita, Papaa Molinga.

Raia huyu wa DR Congo alifunga mabao 11 katika Ligi Kuu Bara akiwa anaitumikia Yanga iliyokuwa na matatizo mengi na kikosi ambacho hakikuwa na nguvu kama kikosi hiki kilichoundwa upya.

Maoni ya wadau wengi wapenda soka waliamini Molinga kwa kuwa alifanya vizuri akiwa na Yanga ambayo haikuwa na wachezaji wengi bora, angekuwa msaada kwa Yanga msimu huu.


Bahati mbaya, viongozi wa Yanga waliokuwa wanafanya usajili, waliamini muarobaini ilikuwa ni kuachana na wachezaji wengi wa kikosi hicho akiwemo mfungaji wao bora wa msimu.


Molinga aliachwa na Yanga yeye mwenyewe akiwa haamini kama uongozi wa Yanga ulifikia kumuacha. Yeye aliona haikuwa sawa lakini hakuwa na namna yoyote ya kuweza kujiokoa na kubaki Yanga.


Moja ya maoni niliyoyatoa wakati huo kwamba Yanga wanapaswa kubaki na Molinga kutokana na uwezo wake wa kufunga mabao licha ya kwamba kikosi cha Yanga wakati huo hakikuwa na nguvu kubwa na kilihitaji marekebisho.


Inawezekana marekebisho yalikuwa makubwa

sana na Yanga walijitahidi kubadilisha mambo,

leo aliyeletwa katika nafasi ya Molinga kwa

maana ya Michael Sarpong ameshindwa, zaidi

ya mechi 15 ana mabao manne na dalili zote

zinaonyesha ataondoka Yanga.


Tuseme sasa ni dakika ya 80 na Molinga bado

anaongoza kwa idadi ya mabao ya kufunga kwa

washambuliaji wa Yanga waliokuwepo msimu

uliopita na hawa wapya katika msimu huu.


Ligi ndio inakwenda ukingoni na unaona kuna

kila dalili utasikia siku moja huenda Molinga au

Herietier Makambo ambaye alikuwepo Yanga

kabla ya Molinga, mmoja wao akirejea kwenda

kuokoa jahazi la kikosi hicho katika ufungaji.


Kuna jambo la kujifunza hapa kwamba wakati

mwingine ni vizuri kuwapa nafasi ambao

ulishawapa nafasi na wakaonyesha namna

fulani ya kufanya vizuri kuliko kwenda

kukimbilia wachezaji wapya ambao hawajawahi

kufanya kazi na wewe hata mara moja.


Maana yake iko hivi, mchezaji ambaye amekuwa na kikosi chako amejifunza utamaduni wa kikosi kwa maana ya ubora na upungufu, namna ambavyo anaweza kupambana na mabeki wa timu kadhaa za Ligi Kuu Bara na pia katika michuano mingine.


Washambulizi wapya wengi wa Yanga wamekuwa hadithi, hata wale viungo washambulizi nao wameshindwa kuwa na msaada mkubwa na kikosi cha Yanga licha ya kwamba wamekuwa na majina makubwa na mbwembwe nyingi.

Kwa maana ya takwimu, Molinga bado ni bora

zaidi ya Carlinhos, bado ni bora dhidi ya Saido

Ntibazonkiza, zaidi ya Abdulrazak Fiston na

bado bora zaidi ya Sarpong. 


Unaona, pekee, Yacouba ndiye anakwenda kumkaribia mkali huyo na katika mechi chache zilizobaki, huenda akafikia idadi ya mabao aliyofunga msimu

uliopita, acha tusubiri huku tukiendelea

kupokea funzo kutoka kwa Molinga.

3 COMMENTS:

  1. Kama inhekuwa yanga in timu yako ingembakisha Hugo ?au kwa sababu so timu yako

    ReplyDelete
  2. Waandishi hawa hawa ndio walisema molinga hastaili kuichezea yanga na kumtolea maneno ya kashfa mwinyi zahera aliyemleta

    ReplyDelete
  3. Hivi ninyi watu Man City Bingwa wa EPL na top striker wao Ana Goli 10 anayeongoza Harry Kane hata top five ilishindikana he hapo tusemeje,? Maana mambo ya sijui kufunga imekuwa issue Sana kwenu.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic