June 4, 2021


 UONGOZI wa Mtibwa Sugar umeweka wazi kwamba kwa sasa mipango yao ni kupambana kupata matokeo chanya kwenye mechi zao ambazo zimebaki.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru amesema kuwa tayari wameanza maandalizi kwa ajili ya mechi zao zilizobaki na wanaamini watafanya vizuri.

"Mtibwa Sugar kweli kwa sasa tumeamua kuona namna gani tutakuwa bora hasa kwa mechi zetu ambazo zimebaki na tunaamini kwamba tutafanya vizuri kupata matokeo chanya.

"Kikubwa ni kwamba kuanzia wachezaji mpaka benchi la ufundi linajua kwamba hatupo sehemu salama kwa sasa ila kila kitu kitakuwa sawa kwani tayari maandalizi yameanza na tuna imani ya kubaki ndani ya ligi," amesema.

Kwenye msimamo Mtibwa Sugar ipo nafasi ya 11 na pointi 34 baada ya kucheza jumla ya mechi 30. 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic