June 4, 2021


 HATIMAYE beki wa kulia wa AS Vita na timu ya Taifa ya DR Congo, Djuma Shabani, amefunguka kuwa yupo tayari kujiunga na Yanga ambayo wapo katika mazungumzo ya mwisho kukamilisha dili lake.

 

Beki huyo anasifika kuwa na uwezo mkubwa wa kuzuia pamoja na kushambulia kwa kasi jambo ambalo limewashawishi viongozi wa Yanga juu ya kumsajili.

 

Akizungumza na Spoti Xtra moja kwa moja kutoka DR Congo, beki huyo alikiri yupo katika mazungumzo na Yanga juu ya kujiunga na timu hiyo.

 

“Ni kweli tupo katika mazungumzo na Yanga, uongozi wangu nimewaeleza ninachohitaji, kama Yanga watakubali basi nitajiunga nao, sitakuwa na shida juu ya hilo kwa kuwa mpira ndio kila kitu kwangu. Uongozi wangu unafahamu kila kitu kuhusu hili, tusubiri tuone,” alisema beki huyo.

 

Spoti Xtra liliutafuta uongozi wa mchezaji huyo ambaye yupo chini ya usimamizi wa Kampuni ya Bro Soccer Management, meneja wake Faustino Mukandila, alisema: “Tupo katika makubaliano ya mwisho na Yanga ya kumsajili Djuma Shabani, katika hili hakuna kingine ambacho naweza kukuambia, labda taarifa za kukamilika kwa usajili wake kujiunga na Yanga.”

9 COMMENTS:

  1. Anakaribishwa, tutampokea airport

    ReplyDelete
  2. Ha ha ha ha ha karibu sana UTO FC,TUTAKUPOKEA AIRPORT KAMA KAWAIDA YETU TENA KWA KITI CHA KIFALME,ILA SIKU YAKUONDOKA UTAONDOKA PEKEAKO HAKUNA ATAKAEKUSINDIKIZA,HUO NDIO UTAMADUNI WA YANGA A.K.A UTO FC,WATAKUCHEKA SANA INAONEKANA HUNA FUTURE BROTHER TAFUTA TIMU.

    ReplyDelete
  3. Namuonea huruma halafu Ana majeruhi huyo hatari

    ReplyDelete
  4. UKIONA VITA WANA MUACHA JUA KUNA KIMEO TAYARI HAPO

    ReplyDelete
  5. Hata ,Kisinda na Mukoko mlisema vile leo mnawavizia

    ReplyDelete
  6. Inauma unayehisi hakubaliki Ana kubalika atauwa kipaji kipi chake unachojua,wewe ?

    ReplyDelete
  7. Well come at Jangwani ur mwananchi now njoo upige KAZI koz mpira ndio Ajira yako popote kambi kikubwa upate changamoto sehemu nyingine achana nao wanao beza koz Yanga ni timu kubwa sana hapa TZ na Africa mashariki na Kati.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic