WAKATI Yanga ikiwa kwenye harakati za mwisho za kukamilisha usajili wa mshambuliaji matata wa Kaizer Chiefs, Mzambia, Lazarous Kambole, uongozi wa Kaizer Chiefs umetoa neno juu ya dili hilo.
Ipo hivi; Inafahamika kuwa, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Yanga, Injinia Hersi Said yupo Afrika Kusini kwa ajili ya kufanikisha dili hilo, baada kumalizana na beki wa AS Vita, Djuma Shabani kwa mkataba wa miaka miwili.
Spoti Xtra linafahamu kila kitu juu ya dili la mshambuliaji huyo ambapo Kaizer wapo tayari kumuachia kutokana na kushindwa kuonesha ubora wake tangu alivyojiunga na timu hiyo mwaka 2019 akitokea Zesco United ya Zambia.
Kambole ameliambiaSpoti Xtra kuwa: “Sina sababu ya kudanganya juu ya hilo, lakini ukweli sijui kitu chochote kinachoendelea.
”Alipotafutwa meneja wa mawasiliano wa timu hiyo, Alpheus Maphosa ‘Vina’ juu ya kuzungumzia hilo, kwanza alionesha ukali akisema: “Siwezi kukubali kuongea na mwandishi iwe kwenye ukweli au uongo, naomba unithibitishie hizo taarifa za tetesi umezitolewa wapi.”
Baada ya kuthibitishiwa taarifa hizo juu ya Yanga kumtaka Kambole, akaibuka na kusema: “Unajua viongozi wa Kaizer wapo bize na mchezo wa nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, sasa kama dili la mchezaji likiwa limekamilika nitakueleza mapema.”
Hakuna kitu hapo, sound tupu
ReplyDeleteMbona Simba mambo yao kimyakimya bila ya kusikia kusikia maporojo ya huyo yupo Congo huyo yupo Zambia na ukitaka uzidi kuwachafuwa na kuwakoroga ni Simba kutamka kuwa wachezaji ambao yanga wanataka kuwatimua ni wa kuwango cha juu sana hivo wana mpango wa kungojea watemwe na wawasajili na hapo ndipo tutapoviona vituko
ReplyDeleteSasa mchezaji wanasema ameshindwa kuonyesha makali alafu nyie ndo mnakomaa nae yanga sijui mmekuwaje, binafsi mm kama shabiki mnanikera sana pyepye nyingi kuliko vitendo mwisho wa siku timu inafanya vibaya badala ya kujadili mnakwama wp mnaanza kutoa taarifa za kupeleka kesi ya Morrison CAS. Sijui mnatuchukuliaje mashabiki kwamba sisi ni mazwazwa
ReplyDeleteKwani lukosa vipi nyie mikia
ReplyDeleteKWANI WE UNASEMAJE? LUKOSA ALISHATIMKIA NORWAY. AMECHEZA MECHI NGAPI?
Deletewewe mwandishi nawe nyau kabisa,habari za mtandaoni ndio unazichukulia kweli,haya sas umeumbuka hao viongozi wa kaizer chief wenyewe hawajui lolote kuhusu kambole kwenda yanga,mnaibukaga tu from know where
ReplyDelete