June 26, 2021


KIERAN Tierney amesaini dili la muda mrefu kuitumikia Klabu ya Arsenal inayonolewa na Kocha Mkuu, Mikel Arteta.

Tierney amesema kuwa ilikuwa ni jambo la haraka kwake kuamua kukubali kubaki ndani ya kikosi cha Arsenal kwa kuwa anaona milango ya mafanikio kwake akiwa ndani ya Emirates.

Beki huyo mwenye miaka  24 amesaini dili la muda mrefu kubaki ndani ya kikosi cha Arsenal kinachonolewa na Kocha Mkuu, Arteta.

Alijiunga na Arsenal msimu wa 2019 akitokea Klabu ya Celtic na amekuwa ni mchezaji muhimu mbele ya Arteta licha ya kwamba amekuwa akisumbuliwa na majeraha ya mara wa mara akiwa amecheza jumla ya mechi 62 na alitwaa taji la FA katika msimu wake wa kwanza.

Beki huyo wa kushoto amesema kuwa anaamini kwamba uwepo wake ndani ya Arsenal ni faida kwake kwa wakati huu na ujao hivyo hana mashaka ya kusaini dili la muda mrefu kwenye kikosi hicho.

Kwa upande wa Arteta amesema kuwa Tierney ni moja ya wachezaji muhimu kwake na anaamini watafanya vizuri jambo ambalo limemfanya ampe dili la muda mrefu.

"Ni mchezaji mzuri anastahili kupewa mkataba mrefu hivyo imani yangu ni kuona kwamba hapo baadaye atafanya kazi nzuri ndani ya Ligi Kuu England," .

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic