MANCHESTER United, wamekubali kutoa kitita cha pauni milioni 77 kwa ajili ya kupata saini ya nyota wa Borussia Dortmund, Jadon Sancho.
Inaelezwa kuwa United wanataka saini ya Sancho ikiwa ni usajili wao wa kwanza na tayari timu yake ya Borussia Dortmund imekubali kumuuza nyota huyo.
Habari zimeeleza kuwa awali Dortmund walikuwa wanahitaji pauni milioni 100 lakini sasa wameshusha mpaka milioni 77.
Awali United ilipeleka ofa kwa mabosi wake kumpata nyota huyo ilikataliwa ila kwa sasa inaelezwa kuwa imejibu na kilichobaki ni kusaini mkataba wa miaka mitano na timu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu England.
0 COMMENTS:
Post a Comment