June 11, 2021


OFISA Habari wa Ruvu Shooting, Masau Bwire amesema kuwa kwa sasa kikosi chao kinapiga hesabu za kuweza kufanya vizuri kwenye mechi zao zilizobaki ikiwa ni pamoja na mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Yanga ambao unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa.

 Kuhusu Edward Manyama ambaye kwa sasa yupo timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, aliyekuwa anatajwa kusaini Simba miaka miwili, Bwire alibainisha kuwa dili hilo halikukamilika na zaidi ya kuwa ni uvumi na anaamini kwamba ni mchezaji ambaye anajielewa. 

Amebainisha kuwa kuna timu ambazo hazina jicho la kutafuta wachezaji. Kwa sasa tayari Manyama ametambulishwa mbele ya Azam FC inayonolewa na Kocha Mkuu, George Lwandamina hivyo msimu ujao wa 2021/22 atakuwa ndani ya Azam FC.

 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic