NYOTA wanne wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, inayonolewa na Kocha Mkuu, Kim Poulsen raia wa Denmark pamoja na wazawa wawili ambao ni Seleman Matola na Juma Mgunda wamewekwa chini ya uangalizi maalumu ili kuweza kurejea kwenye ubora wao.
Juzi wakati Stars ikiendelea kufanya maandalizi yake kwa ajili ya mchezo wa kirafiki unaotambulika na Fifa dhidi ya Malawi unaotarajiwa kuchezwa Juni 13, Uwanja wa Mkapa nyota hao hawakufanya mazoezi ya pamoja na timu.
Ni Salim Aboubakar kiungo wa Azam FC (Sure Boy), Erasto Nyoni beki, John Bocco ambaye ni mshambuliaji na Mzamiru Yassin ambaye ni kiungo na wote ni mali ya Simba walikuwa wakitazama namna Polusen akiwapa mbinu wachezaji wenzao katika Viwanja vya JMK Park.
Akizungumza na Championi Ijumaa, Meneja wa Stars, Nadir Haroub, ‘Canavaro’ alisema kuwa wachezaji hao wapo kwenye uangalizi maalumu kutokana na kusumbuliwa na maumivu madogomadogo.
“Wachezaji ambao hawajafanya mazoezi wao wapo kwenye uangalizi maalumu na hii inatokana na kuwa na maumivu madogomadogo lakini watarudi.
"Tupo imara na tunaamini kwamba tutafanya vizuri hivyo mashabiki waendelee kutupa sapoti kwani kila kitu kinawezekana na wachezaji wanajua majukumu yao," alisema.
hawa wachezaji au TFF WANAJAMBO WANALOFANYA KWENYE HII ISSUE HAWA WACHEZAJI WAKIITWA TIMU YA TAIFA WANAKUA WAGONJWA WAKITOKA HUKO WANAENDA KUCHEZA KNY TIMU YAO BILA KUSINGIZIA UGONJWA. KUNA SIKU WALIWABEBA KWENDA SJUI AFCON WOTE HAWAKUCHEZA ETI WANAUMWA. UJINGA WA MATOLA NA TFF NDIO UNAHARIBU TIMU.
ReplyDelete