June 4, 2021

 


NYOTA wa kikosi cha PSG, Kylian Mbappe amesema kuwa kujilinganisha na mastaa wengine wakubwa duniani ikiwa ni pamoja na Lionel Messi, Cristiano Ronaldo hicho ni kiburi.

Amesema pia wachezaji hao wawili hawalinganishiki kwa kuwa wamevunja sheria zote za takwimu.

Nyota huyo ameweka wazi kuwa ikiwa itakuwa namna hiyo basi atakuwa anawakosea heshima wachezaji hao ambao ni nyota katika ulimwengu wa soka.

Wawili kwa sasa ambao ni Mbappe na staa mwingine wa Borrusia Dortmund, Erling Haaland wanatajwa kuwa watatawala ulimwengu wa soka wakati ujao kwa miaka mingi na kuchukua utawala wa nyota hao wawili ambao muda wao kwa sasa unazaidi kuwaacha taratibu.

Umri wake ni miaka 22 tayari ameshatwaa taji la Kombe la Dunia, mataji manne ya Ligi Kuu ya Ufaransa, (Ligue 1) FA ya Ufaransa mara tatu na Kombe la Ligi mara mbili pamoja na kushika nafasi ya pili ya Ligi ya Mabingwa Ulaya 2020.

Mbappe amesema:"Kama utajiambia mwenyewe kwamba utafanya vizuri zaidi ya hao itakuwa ni kiburi kilichopitiliza, ni kukosa uelewa. Hao ni wachezaji hawalinganishiki wamevunja sheria zote za takwimu,". 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic