June 4, 2021


 UONGOZI wa Klabu ya Yanga umeweka wazi kwamba aliyekuwa mwenyekiti wa timu hiyo, Yusuf Manji ana nafasi ya kurudi ndani ya timu hiyo kwa kuwa hakufukuzwa.

Taarifa zinaeleza kuwa Manji yupo Bongo na hesabu zake kubwa pia ni kurejea katika uwekezaji ndani ya kikosi cha Yanga.

Juni 27, Yanga wanakwenda kwenye mkutano wa mkuu huku moja ya ajenda ikiwa ni mabadiliko na inatajwa kuwa huenda tajiri huyo akaibukia ndani ya mkutano huo.

Katibu wa Yanga, Haji Mfikirwa amesema kuwa Manji hakufukuzwa ndani ya Yanga na akihitaji kurudi atapewa fursa.

"Jambo la muhimu ni kukidhi vigezo na habari njema ni kwamba mfumo wa mabadiliko ya uendeshaji wa klabu unaruhusu wawekezaji, aje tutampokea na si yeye tu, tunaruhusu wawekezaji wengine," .

 

4 COMMENTS:

  1. Kitumbua cha injinia hersi na gsm yake sasa kinaelekea kutiwa mchanga. Nina hakika huko waliko hali si hali

    ReplyDelete
  2. Hawezi kuwekeza huyo,kwani nchi ilishatoka kwenye wapigaji,sasaivi ukidakwa unafilisiwa na kifungo juu,alizoea kupiga huyo enzi za kikwete huu ni msimu wa kazi inaendelea.

    ReplyDelete
  3. Nyie endeleeni kujidanganya na kuwadanganya wengine. I mnazuwa halafu mnajifurahisha. Zaidi ya Mara Mia mmekuwa mkisema Manji anaruji nae kumbe yeye mwenyewe hajatamka na Wala hstaki kulisikia jambo Hilo na nyie mnazidi kumngangania mpaka huyo anaekusaidieni aingie I mitini kwakuwa inaonesha mchango wake hamuuthamini na mnamthamini yule ambae keshskuwacheni mikono na hayupo nanyi

    ReplyDelete
  4. Kuweni waungwana mwachieni Manji apumuwe kwani hivi Sasa yuko anahojiwa na tukuru nanyi mmnamkalia kooni na mnamsahau anaekukwamueni hivi Sasa. Eti mnasherehrkea kwani lino Manji alitamka kuwa anarejea Yanga. Msiache mbachao kwa msala upitao

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic