KOCHA wa zamani wa Manchestrer United ambaye kwa sasa anahudumu ndani ya kikosi cha AS Roma, Jose Mourinho ameibua tena ugomvi wake wa maneno na beki wa klabu ya Manchester United raia wa England, Luke Shaw baada ya kusema kuwa nyota huyo alipiga kona za hovyo katika mchezo wa England dhidi ya Jamhuri ya Czech.
Mourinho alitoa dongo hilo kulenga mchezo wa Jumanne kati ya Jahmhuri ya Czech dhidi ya England ambapo England
waliibuka na ushindi wa bao 1-0, bao lililofungwa na Raheem Sterling.
Mourinho na Shaw wamekuwa katika
bifu la maneno kwa miaka minne sasa, bifu lililotokana na uhusiano mbaya
waliokuwa nao kipindi Mourinho akiwa kocha wa Manchester United.
Katika mahojiano yake na kituo
cha talkSPORT Mourinho amesema: “Kitu kibaya nachoweza kusema ni kuwa kwa mara
nyingine tena England walikuwa na mashambulizi dhaifu ya kona, katika mchezo
dhidi ya Jamhuri ya Czech.
“Mpiga kona alikuwa akipiga kona
mbovu, licha ya kuwa na wachezaji wengi bora ambao wangeweza kutumia mipira ya
kona kwa faida.”
0 COMMENTS:
Post a Comment