KLABU ya soka ya Everton
inaripotiwa kuwa kwenye mipango ya kumsajili nyota wa zamani wa kikosi cha
klabu ya Manchester United anayekipiga ndani ya klabu ya AS Roma, Chris Smalling.
Smalling mwenye umri wa miaka 31, alisaini mkataba wa kusalia moja kwa moja ndani ya kikosi cha Roma katika dirisha lililopita la usajili wa kiangazi, baada ya kucheza kwa mkopo wa msimu mmoja ndani ya Roma, anatajwa kuwa hayuko kwenye mipango ya kuuzwa na wababe hao wa Italia.
Lakini Roma wameeleza kuwa tayari
kusikiliza ofa ya kumuuza kiungo huyo waliyemnunua kwa Euro Milioni 18, lakini
kwa sharti la kutafuta mbadala wake kabla ya kufanya uamuzi huo.
0 COMMENTS:
Post a Comment