June 18, 2021


 KIKOSI cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes, kesho Juni 19 kina kibarua cha kusaka pointi tatu muhimu mbele ya Polisi Tanzania. 

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza majira ya saa 10:00 jioni.

Kwa mujibu wa Meneja wa Simba, Patrick Rweyemamu amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo wao huo.

Mchezo uliopita walipokutana Uwanja wa Mkapa, ubao ulisoma Simba 2-0 Polisi Tanzania hivyo utakuwa ni mchezo wa kisasi kwa Polisi Tanzania.

Kwa upande wa Polisi Tanzania inayonolewa na Kocha Mkuu, Malale Hamsini imeweka wazi kwamba inahitaji pointi tatu pia muhimu.

Kwenye msimamo wa ligi, Simba inaongoza ligi ikiwa na jumla ya pointi 67 baada ya kucheza mechi 27 inakutana na Polisi Tanzania iliyo nafasi ya 8 na pointi 41.

2 COMMENTS:

  1. Wewe mwandishi boya kweli, umeng'ang'ania mchezo uko moshi wakati timu ziko mwanza? Tumia muda japo kidogo kuhariri report zako, inaonekana hauko makini ni mtu wa kucopy na kupaste.

    ReplyDelete
  2. Yani waandishi wa humu wanazidiwa na wasomaji... Unasoma taarifa unaona kabisa mwandishi hana anachojua

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic