June 4, 2021


 UONGOZI wa Yanga umeweka wazi kwamba hauhitaji maandalizi kwenye mchezo wao ambao utawahusu watani wao wa jadi Simba hata wakiamshwa usiku wataingia uwanjani kucheza bila mashaka.

Mchezo wao wa awali ambao ulipaswa kuchezwa Uwanja wa Mkapa uliyeyuka baada ya watani hao wa jadi kueleza kuwa wanafuata kanuni kutokana na Bodi ya Ligi Tanzania kubadili muda ghafla ikiwa ni masaa machache kabla ya mchezo huo. 

Kufuatia kuahirishwa kwa mchezo huo Bodi ya Ligi ilipanga mchezo mwingine kuchezwa Julai 3 na Yanga kupitia kwa Ofisa Habari, Hassan Bumbuli aliweka wazi kwamba wana mechi nne ambazo zimebaki na hizo watawekeza nguvu kubwa kwa maandalizi.

Bumbuli amesema:"Mchezo wetu sisi dhidi ya Simba hauhitaji maandalizi hata tukiamshwa usiku sisi tunacheza na hata tukiamka asubuhi sisi tunacheza hatuna tatizo nao.

"Nilisema kwamba tumebakiwa na mechi nne ambazo ni fresh kwa sababu hizo zipo kwenye ratiba na hata mwalimu anajua kwamba hizo zipo na tutafanya vizuri.

"Kuhusu mechi ya Simba, Julai 3 hiyo ipo kama ambavyo imepangwa na Yanga haijatoa tamko kuhusu mechi hiyo hivyo kilichopo ni kuona kwamba tunajiandaa. Ule ni mchezo wa kiporo hauna mambo mengi tupo tayari," amesema. 

7 COMMENTS:

  1. Huo ujinga awaaminishe utopolo. Alikuwa anamaanisha kweli wanapanga kukimbia tena ila wamechungulia adhabu ambayo o gewashukia wanageuza maneno. Kama mechi na simba ukiamshwa unacheza kulikoni tar 8 mlikimbia, ujinga mzigo.

    ReplyDelete
  2. Mkiamshwa usiku mtasema ni kinyume na kanuni. Taarifa imekuja mapemaa, jiandaeni na Julai 3, sio usiku

    ReplyDelete
  3. kumbe wenye akili na wanao ongea sawa na Masau Bwire wengi! Kama timu yenu ilikataa kucheza saa moja, hivi kweli itacheza usiku?

    vipi kesi ya Morrison imefika wapi...maana jana anahusika na kasaidia magoli mawili. tupeni update

    ReplyDelete
  4. Kutapatapa kwa Hali ya juu kabisa. Ukiwa msemaji wa taasisi kubwa kama Yanga, weledi, umakini na ufahamu unahitajika. Sio kwa uropokaji huu. Ndo maana narudia kusema Yanga Haina viongozi makini.

    ReplyDelete
  5. Hata tukiamshwa usiku na Morrison tupo tayari kwani mpaka Sasa ubingwa bado hauna mwenyewe kwani tutashinda mechi zote zilizobakki na Simba kushindwa zote zilizobakki na hiyo ndio hesabu zetu

    ReplyDelete
  6. Sasa wanamtaka Manji tu wengine hawatakiwi

    ReplyDelete
  7. Ni funzo kwa fff inayopenda kupindisha utaratibu kwa kusikiliza kila maombi ya mikia baada ya kuchungulia kipondo.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic