July 15, 2021

 


MATAJIRI wa Dar, Azam FC wamegawana pointi mojamoja na Simba katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Azam Complex. 



Dakika 90 zimekamilika kwa ubao kusoma Azam FC 1-1 Simba na ule wa mzunguko wa kwanza ilikuwa Simba 2-2 Azam FC.


Azam FC wakiwa Uwanja wa Azam Complex walianza kupachika bao la kuingoza dk ya 43 kupitia kwa mzawa Idd Seleman, 'Nado'.


Bao hilo lilidumu mpaka kipindi  ha pili likiwa ni bao la 10 kwa Nado kiungo mshambuliaji wa Azam FC. 


Kipindi cha pili Meddie Kagere dk 84 aliweka mzani sawa na kufanya ngoma iwe ngumu kwa timu zote mbili ambapo Azam FC inagawana pointi mojamoja mbele ya Simba.


Kipindi cha pili Azam FC walipata nafasi mbili za dhahabu mwisho wa siku wakakwama kupata ushindi ambapo Ayoub Lyanga alitaka kupachika bao mwisho wa siku akakamwa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic