July 15, 2021

 WACHEZAJI wa Azam FC leo Julai 15 wamewapigia makofi mabingwa wa Ligi Kuu Bara,  Simba katika mchezo wao ambao wanacheza leo Uwanja wa Azam Complex. 



Kanuni zinaeleza kuwa bingwa akipatikana wakati ligi inaendelea na anamechi mkononi atapigiwa makofi kwa kumtengenezea gwaride la heshima, (guest of honour).


Simba ni mabingwa wa ligi wakati wakiwa wamebakiza mechi mbili mkononi hivyo katika mechi ya leo Uwanja wa Azam Complex wamepigwa makofi.


Pointi zao kibindoni ni 79 zimewafanya watangazwe kuwa mabingwa huku Azam FC ikiwa nafasi ya tatu na pointi 64.


Itakabidhiwa taji katika mchezo wa Julai 18 mbele ya Namungo FC, Uwanja wa Mkapa.

2 COMMENTS:

  1. Hui ni mfano wa kuigwa kwa timu zetu zote, tukubali utaratibu. Ingekuwa timu zingine za akina burundi bumbuli fc ungesikia kelele na zengwe linaamka

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kama ambavyo ingekuwa kinyume chake. Tofautisha Azam na haya mazimwi mawili

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic