MABOSI wa Dar, Klabu ya Azam FC imemtambulisha nyota mpya leo Julai 19 kwa mashabiki wao.
Ni mshambuliaji wa kimataifa wa Zambia, Rodgers Kola, kwa usajili huru akitokea Zanaco ya huko Zambia.
Taarifa iliyotolewa na Azam FC imeeleza kuwa mshambuliaji huyo mzoefu, mrefu na mwenye umbo kubwa, amesaini mkataba mbele ya Ofisa Mtendaji Mkuu, Abdulkarim Amin 'Popat', utakaomfanya kudumu ndani ya viunga vya Azam Complex hadi mwaka 2023.
Kola anakuja kuongeza nguvu kwenye safu yetu ya ushambuliaji, kuanzia msimu ujao 2021/2022.
Aidha Kola ambaye wakala wake ni Nir Karin, akiwa Zanaco msimu uliopita, alifunga jumla ya mabao 14 katika mashindano mbalimbali nchini Zambia.
Azam mwakani atatisha
ReplyDeleteHao mbwembwe zao ni kama za mwendokasi kujaza mabasi kibao yard lakini barabarani kero tupu hakuna mafanikio yoyote
DeleteHahaaaaaaa..
DeleteAzam FC hata wachukue kikosi kizima cha Real Madrid hawanaga maajabu
ReplyDeleteUnauhakika na usemayo
Deletehongera sana azam fc kwa usajili huo,ngoja ligi zikianza tutaambizana
ReplyDelete