July 19, 2021


 YANGA imepania kufanya kweli katika usajili msimu huu, hiyo ni baada ya kukamilisha usajili wa Shabani Djuma, sasa klabu hiyo ipo katika mazungumzo ya mwisho na kipa wa Aigle Noir ya nchini Burundi, Erick Johola.

 

Johola, licha ya kucheza katika Ligi Kuu ya Burundi, lakini ni Mtanzania ambapo kipa huyo alidaka katika mchezo wa kilele cha Wiki ya Mwananchi msimu uliopita na katika mchezo huo licha ya kuonyesha kiwango kikubwa, Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 2-0.

 

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Yanga, Injinia Hersi Said, aliweka wazi kuwa nchini Burundi katika Klabu ya Aigle Noir, wametengeneza urafiki mzuri sana kwa kuingia makubaliano ya baadhi ya mambo, hivyo watu wasishangae kuona wanasajili mchezaji kutoka katika klabu hiyo ambaye tayari walishamfanyia skauti na wamevutiwa naye.

 

“Burundi tumetengeneza urafiki mzuri na Klabu ya Aigle Noir na tumekubaliana katika ushirikiano wa baadhi ya mambo na tumevutiwa na mchezaji mmoja, kwa hiyo msishangae kuona kuwa tumesajili mchezaji kutoka hapo.

 

"Tumefanya skauti ya kutosha nchini Burundi, kama ambavyo mnafahamu ni nchi jirani na baada ya mchezo wetu dhidi yao tulikubaliana kushirikiana katika mambo ya maendeleo ambayo ni pamoja na haya ya usajili,” alisema kiongozi huyo.

 

Akizungumza na Championi Ijumaa, Johola alikubali kuwa yupo katika mazungumzo na uongozi wa Yanga ambao unahitaji huduma yake huku yeye akiweka wazi kuwa yupo tayari kujiunga na Yanga iwapo watafikia katika makubaliano mazuri.

 

“Ni kweli nipo katika mazungumzo na uongozi wa Yanga, wao wameonyesha kuhitaji saini yangu ili niweze kuitumikia, hivyo ndivyo ninavyoweza kukuambia na kama mazungumzo yetu ambayo bado hajakamilika yatafanikiwa kukamilika, basi nitakuwa tayari kujiunga na Yanga,” alisema kipa huyo.


Leo Julai 19 dirisha la usajili limefunguliwa na linatarajiwa kufungwa Agosti 31.

4 COMMENTS:

  1. Tatizo kubwa la Yanga wanatamani wachezaji wazuri ila pesa ya kusajili hawana, wao kazi yao ni kuongea ongea tu, utasikia tupo kwenye mazungumzo, mwisho wa siku mchezaji huyo huyo anasajiliwa na Simba au Azam. Umaskini ni mateso makubwa sana.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Heri yako wewe tajiri wa mkopo

      Delete
    2. Tulia wewe mjukuu Wa Mwamedi,subiri Mo aongee sio wewe

      Delete
  2. Mpira ndivyo ulivyo mama,kama utaweza ichukue wewe uidhamin,punguza wivu na ongeza mapenzi kwenye mpira ila uwe na kipimo kwenye kushabikia timu maana usipokua na mizani,utakera watu kwa mapovu yako yasiyo na nguvu,ningekushauri tumia nguvu nyingi kujenga maisha bora ya familia yako,inawezekana ikaja kukusaidia baadae kuliko kupiga porojo hapa.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic