July 21, 2021

BAADA ya juzi Jumatatu kufanikiwa kutupia bao lake la pili ndani ya kikosi cha klabu ya Genk, mshambuliaji kinda wa kimataifa wa Tanzania, Kelvin John ‘Mbappe’ ametamba kuwa malengo yake ni kuhakikisha anapata nafasi ya kucheza kwenye kikosi cha kwanza cha timu ya wakubwa ya Genk.

Mbappe alijiunga na kutangazwa rasmi na Genk Julai 25, mwaka huu kwa mkataba wa miaka mitatu ambao utamuweka ndani ya timu hiyo mpaka mwaka 2024, huku ikielezwa kuwa nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta alikuwa sehemu kubwa ya ushawishi wa usajili huo.

Katika michezo miwili iliyopita nyota huyo amefanikiwa kuifungia KRC Genk ya vijana mabao mawili.

Akizungumzia mipango yake, Mbappe amesema: “Najisikia furaha kuwa sehemu ya kikosi cha klabu ya Genk, nashukuru kwa ushirikiano ambao nimekuwa nikiupata kutoka kwa wenzangu ambao ni wazi umenifanya nizoee mazingira mapema, na kufanya vizuri katika michezo miwili iliyopita.

“Malengo yangu ni kuhakikisha najitahidi kuonyesha uwezo mkubwa ili niweze kumshawishi kocha aweze kunipa nafasi kwenye kikosi cha kwanza cha timu ya wakubwa.”

6 COMMENTS:

  1. Acheni ujinga Mbape ndo mini? Ikitokea Genk wanacheza na PSG Mbape atakuwa yupi?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Usi laumu wenzako FANYA juuu na WEWE upate chako juuu

      Delete
  2. Ujinga wanini na WEWE , fanikiwa na weqebusifike sio kulaumu wenzako

    ReplyDelete
  3. Mwandishi wa hii habari ni kiazi. Eti Kelvin John alisajiliwa ghent julai 25 mwaka huu.

    ReplyDelete
  4. 25 julai 2021, et Kelvin kasajiliwa

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic