ZIKIWA zimepita siku chache baada ya msimu wa Ligi Kuu Bara 2020/21 kumalizika, imebainika kwamba msimu ujao wa 2020/21 unatarajiwa kuanza kutimua vumbi rasmi mwezi Septemba mwaka huu.
Ligi Kuu Bara ilifikia tamati Jumapili iliyopita, ambapo michezo tisa ya timu zote 18 ilipigwa, na kushuhudia klabu ya Simba ikikabidhiwa ubingwa wa nne mfululizo huku klabu za JKT Tanzania, Gwambina, Ihefu na Mwadui zikishuka daraja.
Kupitia ligi ya msimu huu, klabu
nne zimefanikiwa kukata tiketi ya kushiriki michuano ya kimataifa msimu ujao
ambapo, Simba na Yanga zitashiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, huku
Azam na Biashara United zikishiriki michuano ya kombe la Shirikisho.
Akizungumzia ratiba hiyo, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), Almas Kasongo, amesema: “Msimu wa Ligi Kuu Bara tunatarajia uanze mwezi Septemba mwaka huu, ingawa mpaka sasa bado hatujapanga tarehe rasmi ya kuanza kwa ligi.
Wakati ligi ikitarajiwa kuanza
mwezi Septemba, juzi Jumatatu, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), lilitangaza
kufunguliwa rasmi kwa dirisha la usajili ambalo litafungwa Agosti 31, mwaka
huu.
Ushauri ligi ianze mwezi was nane mwishoni lisije likajirudia ya msimu wa 2018/2019 timu hazikuwa na match fitness nazilikuwa nne zikatolewa zote mapema. We have to take as a precaution.
ReplyDeletekel kabisa
DeletePlot 89 block 25 makao makuu majengo timu zilizochuwa champion ahly na conferedarion zimebadilika sana mchezoni
ReplyDelete