July 20, 2021




 RASMI leo Julai 20 nyota wa timu ya Ruvu Shooting amemalizana na mabosi wa Azam FC akiwa ni mchezaji huru baada ya dili lake la miezi sita kumeguka ndani ya kikosi hicho.


Awali nyota huyo alikuwa anatajwa kumalizana na Simba ambao waliamua kuwavutia waya mabosi wa Azam FC ili wawaachie beki huyo ila ilielezwa kuwa dili hilo lilibuma.

Kupitia Ukurasa rasmi wa Instagram wa Azam FC umeandika namna hii:"Tunayofuraha kuingia mkataba wa miaka miwili na beki kisiki wa kushoto wa kimataifa wa Tanzania, Edward Manyama, kwa usajili huru akitokea Ruvu Shooting.


"Mkataba huo utamfanya Manyama kuhudumu ndani ya viunga vya Azam Complex hadi mwaka 2023. Manyama ni mmoja wa mabeki wa kushoto wanaoendelea kufanya vizuri kwenye ligi yetu, ingizo lake ndani ya kikosi chetu ni katika kuimarisha zaidi eneo hilo.

"Huo ni usajili wa tatu katika kikosi chetu kuelekea msimu ujao, baada ya awali kuwasaini nyota wa kimataifa wa Zambia, kiungo mshambuliaji, Charles Zulu na mshambuliaji, Rodgers Kola," .

7 COMMENTS:

  1. Hovyoo vipi beki wa simba? Sawa na kujitekenya mwenyewe na kujichekesha mwenyewe.

    ReplyDelete
  2. Mi nilifikiri katoka Simba,kumbe katoka Ruvu!waandishi andikeni kilichojiri na sio kisichojiri

    ReplyDelete
  3. Hawa waandishi huwa wanapenda kuona matusi ya wasomaji kutokana na uandishi kilaza walionao

    ReplyDelete
  4. Huyu si walimsajiri kipindi kile yuko ma timu ya taifa, vipi tena anasajiriwa leo?

    ReplyDelete
  5. Huyo ndiye beki wa simba acheni ushamba kuwa makini na taaluma yenu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic