NDANI ya msimu wa 2020/21 eneo la kucheka na nyavu kwa kiasi kikubwa wazawa wameweza kujitahidi kwa kufanya vizuri.
Ni John Bocco anayekipiga ndani ya Simba kwenye chati yupo namba moja akiwa ametupia mabao 16 na ana pasi mbili za mabao kibindoni. Timu yake imefunga jumla ya mabao 78.
Yupo mwingine kutoka Azam FC, Idd Seleman, ‘Nado’ ambaye yeye ametupia jumla ya mabao 10, katika mabao hayo amewatungua Simba nje ndani kila walipokutana kwa msimu huu ule mchezo wa kwanza, Uwanja wa Mkapa na ule wa pili Uwanja wa Azam Complex.
Azam FC ipo nafasi ya tatu ina pointi 68 ikiwa imefunga jumla ya mabao 53 baada ya kucheza jumla ya mechi 34.
Mzawa mwingine mkali wa kucheka na nyavu ni Danny Lyanga ambaye yupo zake JKT Tanzania akiwa ametupia mabao 10. Licha ya kuwa na mabao mengi timu yake imeshuka.
Ipo nafasi ya 15 na pointi 39 na imefunga jumla ya mabao 34. Inaungana na Mwadui FC ambayo ilianza mapema kushuka ligi kwa msimu wa 2020/21.
0 COMMENTS:
Post a Comment